Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza juisi cha BAKHRESA FOOD PRODUCTS LIMITED, Naimesh Kansara, akiwaonesha timu ya wapigapicha waliokuwa katika safari ya upigaji picha za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC PHOTO SAFARI), walitembelea kiwanda hicho, ujazo mpya wa boksi za juisi, ambazo Kampuni hiyo itaanza kuzizalisha mapema mwakani. Timu hiyo ya wapigapicha, ilitembelea kiwanda hicho kwakuwa Bakhresa ni Moja ya Makampuni ya Kitanzania ambayo, yanafanya biashara zake pia katika nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
| Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza juisi cha BAKHRESA FOOD PRODUCTS LIMITED, Naimesh Kansara, akiwa amekaa na baadhi ya pakiti za juisi zinzotengenezwa na kiwanda hicho, wakati timu ya wapigapicha waliokuwa katika safari ya upigaji picha za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC PHOTO SAFARI), walitembelea kiwanda hicho Dar es Salaam leo. |
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho, Manka akionesha pakiti hizo mpya za juice za ladha mbalimbali hadi juisi ya dafu ambazo zitaanza kuzalishwa mwakani.
Juisi za ujazo tofauti, zikiwa katika mpangilio unaovutia
Mfanyakazi wa Kiwanda chya Juice za AZAM akiwa kazini katika uzalishaji.
Kiongozi wa Msafara wa Wapigapicha za EAC, ambaye ni Mtaalam wa Masuala ya Vyombo vya Habari, Sukhdev Chhatbar (kushoto), akizungumza jambo na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho cha Juisi, Naimesh Kansara.

No comments:
Post a Comment