TANGAZO


Tuesday, September 25, 2012

TAWLA yafanya mkutano wa kujadili migogoro ya ardhi

Baadhi ya wadau wakiwa na wanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA), wakiwa katika mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti kuhusu migogoro ya ardhi inawakabili wanawake, jijini Dar es Salaam leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kupatia matokeo ya utafiti uliofanyika katika Mkoa wa Dare s Salaam na Tanga, uliofadhiliwa na TAWLA.

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya ya Kinondoni, Charles Mnzava (kulia), akichangia mjadala, jijini Dar es Salaam leo, kuhusu matokeo ya utafiti wa migogoro ya ardhi inawakabili wanawake . Mkutano huo ulikuwa na lengo la kupatia matokeo ya utafiti uliofanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga uliofadhiliwa na TAWLA. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi wilayani Ilala, Raphael David.
 
Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Patricia Fikirini (kulia), akitoa maoni yake, jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mjadala kuhusu matokeo ya utafiti wa migogoro ya ardhi, inayowakabili wanawake. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kupatia matokeo ya utafiti uliofanyika katika Mikoa wa Dar es Salaam na Tanga na kufadhiliwa na TAWLA. Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mstaafu, Eusebia Munuo.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA), Aisha Bade (kulia), akitoa ufafanuzi jijini Dar es Salaam leo, kuhusu matokeo ya utafiti wa migogoro ya ardhi inayowakabili wanawake. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kupata matokeo ya utafiti uliofanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga, uliofadhiliwa na TAWLA. Kushoto ni Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Ilala, Tarsua Kesoka. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment