TANGAZO


Monday, September 24, 2012

Gerrard awapongeza mashabiki wa Liverpool, Man Utd


LIVERPOOL, England

“Kulikuwa na mengi yaliyosemwa kuhusu mashabiki wa pande zote mbili na utulivu uliooneshwa nao katika tukio hili na mchezo kwa ujumla ulikuwa ni kitu cha kuvutia kinachostahili pongezi”

KIUNGO mahiri wa Liverpool, Steven Gerrard, amewapongeza mashabiki wa soka wa klabu yake na wale wa Manchester United kwa hisia njema walizoonesha katika mechi kati ya timu hizo kwenye Uwanja wa Anfield.

Liverpool ilikuwa mwenyeji wa mahasimu wao kwa mara ya kwanza tangu kutolewa kwa ripoti huru kuhusiana na maangamizi ya Hillsborough, ambayo iliwasafisha mashabiki wa klabu hizo na kuhusika moja kwa moja na vifo vya wenzao 96 vilivyotokea Aprili 1989.

Kulikuwa na shaka ya kuwapo kwa mtifuano baina ya mashabiki wa pande mbili hizo hasimu licha ya miito ya kuzitaka kudumisha amani, lakini badala yake mashabiki wa United wakaungana na Kop kutoa heshima kwa marehemu hao.

Gerrard nahodha wa Liverpool, alisema: “Kulikuwa na mengi yaiyosemwa kuhusu mashabiki wa pande zote mbili na utulivu ulioneshwa nao mchezoni ulikuwa kitu cha kuvutia kinachostahili pongezi.”

Mabosi wa klabu hizo, Brendan Rodgers na Sir Alex Ferguson waliungana kwa pamoja kuwapongeza mashabiki hao, ambapo Fergie alisema: “Liverpool walifanya kazi nzuri, mashabiki wao walikuwa na hisia kali na sidhani kama kuna malalamiko katika hilo.

“Ilikuwa mshikamano wa aina yake, Bobby Charlton akitoa shada la maua kwa Ian Rush na kuthibitisha kwamba klabu hizi mbili zinaweza kufanya mambo makubwa kwa umoja,” alisema Fergie.

Rodgers kwa upande wake akaongeza: “Kama klabu kinara zinazopigiwa mfano katika soka la hapa, tuna wajibu, kimaadili na kijamii, ili kuongoza – na nadhani kwa pamoja tumefanya hivyo leo.”

Kwa upande wa Jeshi la Polisi huko Merseyside, lilitoa tamko kupitia ukurasa wao wa kijamii wa Twitter na kuandika: “Shukrani za dhati kwa seti ya mashabiki wa timu zote kwa kuheshimu tukio hili. Walionesha tabia njema na kuzifanya klabu zao kujivunia.”

No comments:

Post a Comment