Meneja wa vipindi wa Clouds Tv, Wasiwasi Mwambulambo (kulia), akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Bibi Bomba, jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa Mawasiliano wa benki ya NMB, Josephine Kulwa (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Bibi Bomba. Kulia ni Meneja wa vipindi wa Clouds Tv, Wasiwasi Mwambulambo.
Washindi wa Bibi Bomba, kutoka kushoto ni Mshindi wa kwanza, Veronica Mpandala Matia kutoka Mikocheni, jijini Dar es Salaam, Anna Said mkazi wa Mikocheni na Nasra Mohamed Abdullah mkazi wa mjini Zanzibar.
Meneja wa Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa (kulia), akibidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni moja, mshindi wa tatu wa shindano la Bibi Bomba, Nasra Mohamed Abdullah kutoka Zanzibar katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Katikati anayeshuhudia ni Meneja wa vipindi wa Clouds Tv, Wasiwasi Mwambulambo.
Meneja wa Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa (kulia), akimbidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni tatu mshindi wa pili wa shindano la Bibi Bomba, Anna Said mkazi wa Mikocheni A, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Katikati anayeshuhudia ni Meneja wa vipindi wa Clouds Tv, Wasiwasi Mwambulambo.

No comments:
Post a Comment