TANGAZO


Sunday, September 30, 2012

Rais Mstaafu Mzee Mwinyi awakabidhi Kwadelo tangi la maji, kitanda cha kujifungulia


 
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omari Kariati akimsalimia mke wa Rais mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti, nyumbani kwao, Mikocheni jijini Dar es Salaam, kabla ya hafla ya wananchi wa Kata hiyo kukabidhiwa tangi la maji na kidanda cha kujifungulia akina mama, iliyofanyika nyumbani hapo leo.
Diwani Kariati, akiongozana na Rais mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mama Sitti, kwenda eneo la tukio la kukabidhi vifaa hivyo.
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa,  Omari Kariati, akiangalia mmoja ya miembe ya kisasa uliopo nyumbani kwa Rais mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Baadhi ya akinamama wa Kwadelo, wakiwa kwenye viwanja vya shughuli ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa, akimshukuru Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia) kwa kutokana na kuwakaribisha nyumbani kwake kukamilisha hafla hiyo. Katika shughuli hiyo ya kuwakabidhi wana-Kwadelo tangi la maji la sh. 650,000 na kitanda cha kujifungulia kina mama pia Mzee Mwinyi alimpatia sh. 200,000 kijana  aliyemuahidi kwa ajili ya kukamilisha masomo yake ya ualimu Ununio. Katikati ni Mkewe Mama Sitti.
Kisha mzee Mwinyi na mkewe wakasongea pamoja na waalikwa pahala vilipokuwa vitu vya kukabidhi. Hapa anakabidhi kitanda.
Kwa furaha baada ya kukabidhiwa, mama mmoja wa Kwadelo akakifanyia majaribio kidogo kitanda hicho.
Mzee Mwinyi akikabidhi tangi la lita 5000 kwa Mwadham Msami (kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerereng'ombe, Kwadelo. Diwani Omari Kariati (wa pili kulia), akishuhudia tukio hilo.
Baada ya kurejea meza kuu, Mzee Mwinyi akakabidhi sh. 200,000 kwa kijana, Kassim Omar kwa ajili ya kumalizia masomo yake ya ualimu Chuo cha Ununio, Bagamoyo.
Mzee Mwinyi akazungumza ya moyoni kuwausia wana Kwadelo na Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.
Picha za pamoja na Mzee mwinyi zikapigwa kwa makundi ya wananchi wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
Hawa ni kina mama wa Kwadelo wakiwa na Mzee Mwinyi
Na kina Baba wakachangamkia
Vijana wa Kwadelo wakiwa nyuma ya Mzee Mwinyi katika picha ya pamoja
Hawa pia ni vijana wa Kwadelo kati ya 50 wanaofanya shughuli zao jijini Dar, waliojitolea kwenda kulima katika kata hiyo.
Waandishi nao wakatumia fursa hiyoo adhimu kupigapicha na Mzee Mwinyi.
Hapa pia ni waandishi wakichangamkia fursa hiyo.
Mama Sitti akiwakaribisha wageni mwishoni mwa shughuli.
 
Wageni wakipata chai wakati wa shughuli hiyo. (Picha zote na mdau wetu)
 

No comments:

Post a Comment