TANGAZO


Monday, August 13, 2012

Waandishi Mara wafunzwa kuandika habari za afya

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara wakiwa kwenyenye mafunzo ya uandishi wa habari za afya. Mafunzo hayo ya siku nne yanaendeshwa na chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa Mara (MRPC), kwa ufadhili wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habri Tanzania (UTPC), mjini Musoma leo. (Picha zote na Ahmed Makongo)



Baadhi ya waandishi wa hao wakiwa katika mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mara (MRPC), kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), mjini Musoma leo.


Waandishi Mara wapata mafunzo juu ya uandishi wa habari za Afya


Na Ahmed Makongo, Musoma;
Agosti 13, 2012;

JUMLA ya waandishi wa habari 18 wa vyombo mbalimbali kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara, wananshirki mafunzo ya siku nne juu ya uandishi wa habari za afya, yanayofanyika mjini Musoma.
Kwa mjibu wa Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mara (MRPC), Beldina Nyakeke, alisema kuwa mafunzo hayo, yanaendeshwa na MRPC kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Nyakeke alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa huo, ili kuweza kupata upeo wa kufuatilia na kuandika kwa kina juu ya habari za afya.
“Mafunzo haya yanaendeshwa na MRPC kwa ufadhili wa UTPC, yakiwa na lengo la kuwajenge uwezo waandishi hao, ili waweze kupata upeo wa kufuatilia na kuandika kwa kina habari za afya” alisema Nyakeke.
Mwezeshaji mmoja kwenye mafunzo hayo yaliyoanza jana jumatatu, Dk. Ahmed Twaha, alisema kuwa waandishi hao wataelimishwa kwa kina kuhusu uandishi wa habari za afya, ambapo watapata uelewa, ikiwa ni pamoja na kuboresha maarifa na stadi za uandikaji wa taarifa za afya.
Dk. Twaha ambaye ni bingwa wa afya ya jamii, alisema kuwa waandishi hao pia watakwenda kujifunza kwa kutembelea hospitali na vituo vya afya, ambapo wataangalia changamoto mbalimbali na kuziandikia makala, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii inayowazunguka kwa kutumia vyombo vyao vya habari.
“Pia baada ya mafunzo ya humu ndani, mtatembelea kwenye hospitali na vituo vya afya na kuangalia changamoto mbalimbali na kisha mtaandika habari” alisema Dk. Twaha.
Alisema afya kwa jamii inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na jamii kutowapatia lishe bora watoto wao, kwa kubagua vyakula vyenye lishe na kusababisha utapiamulo kwa watoto, ambapo amesema ni jukumu la waandishi wa habari kutumia kalamu zao kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya lishe bora.
Aidha, aliwataka waandishi wa habari kuelimisha jamii juu ya afya ya msingi, ili jamii iweze kuchukua hatua madhubuti kukabilia na changamoto mbalimbali za magonjwa.

No comments:

Post a Comment