Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' na wenzake wakiangalia baadhi ya CD na DVD za filamu na michezo ya kuigiza ambazo wajanja wamekuwa wakizirudufu na kuziuza kinyume na matakwa ya wamiliki wake.
Msanii wa Filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati walipokuwa wanatoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuwa wameungana kupambana na maharamia wa kazi zao za sanaa. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na msanii Muhsin Awadh 'Mr Chen'.
Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, juu ya wizi mkubwa uliotokea hivi karibuni uliofanywa na Kampuni ya Steps Entatainment kwa kushirikiana na wasanii wenyewe na kudai kuwa tabia hii ikomeshwe kwa maharamia wa kazi za wasanii. Kulia ni Msanii Vicent Kigos 'Ray' na Mwenyekiti wa Shilikisho la Filamu Tanzania 'TAFF' Simon Mwakifwamba.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo baada ya wasambazaji kuungana na wasanii kwa ajili ya kutoa tamko la kupambana na Maharamia wa kazi za sanaa. Kushoto ni msanii Muhsin Awadhi na Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' (Picha zote na www.burudan.blogspot.com)

No comments:
Post a Comment