TANGAZO


Friday, August 10, 2012

Waziri wa Fedha Dk. Mgimwa afungua mkutano wa baraza la wafanyakazi


  Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha leo, jijini Dar es Salaam. Katika salama zake kwa wafanyakazi amewaagiza kuweka mfumo mzuri wa ulipaji mishahara ili kuepuka malipo kwa watumishi hewa na kuongeza kuwa watakaoshiriki katika malipo hewa watachukuliwa hatua kali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanyakazi wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijjah akimkaribisha Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa (hayupo pichani), ili afungue mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo mara baada ya ufunguzi wa mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Tiganya Vincent - MAELEZO)

No comments:

Post a Comment