Mkuu wa Huduma za Kibenki wa BancABC, Mwalimu Zubery, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wadhamini wa michuano ya BancABC Sup8r 2012, walipokuwa wakitangaza ratiba na timu zikazochuana katika hatua hiyo, michezo itakayofanyika kesho, Uwanja wa Taifa jijini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Boni Nyoni na kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki wa BancABC, Mwalimu Zubery na kulia ni msemaji wa Simba, Ezekile Kamwaga.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kocha wa timu ya Jamhuri ya Pemba, Ameir Machano Haji 'Chua', Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Boni Nyoni na Mkuu wa Huduma za Kibenki wa BancABC, Mwalimu Zubery.
Baadhi ya waandishi wa habari, viongozi wa timu zitakazochuana katika hatua ya nusu fainali na Maofisa wa BancABC, wakiwa kwenye mkutano huo, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wakuu wa Simba, Jamhuri, Mtibwa, Azam FC, BancABC na TFF katika mkutano huo leo.
Kocha wa timu ya Jamhuri ya Pemba, Ameir Machano Haji 'Chua', ambaye timu yake itapambana na Mtibwa katika hatua ya nusu fainali ya kwanza mchana kesho, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wadhamini wa michuano ya BancABC Sup8r 2012, walipokuwa wakitangaza ratiba na timu zikazochuana katika hatua hiyo, michezo itakayofanyika kesho, Uwanja wa Taifa jijini. Kutoka kushoto, wapili ni Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Boni Nyoni, Mkuu wa Huduma za Kibenki, Mwalimu Zubery na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah.
Msemaji wa Simba, Ezekile Kamwaga, akizungumza kwenye mkutano huo, kuelezea matayarisho ya kikosi cha timu yao kitakachoshuka dimba la Uwanja wa Taifa, jioni kupambana na Azam FC katika nusu fainali ya pili kesho. Kushoto ni viongozi wa BancABC na Katibu wa TFF, Angetile Osiah. Mbele yao ni kombe atakalokabidhiwa bingwa wa michuano hiyo.
Baadhi ya viongozi wakuu wa Simba, Jamhuri, Mtibwa, Azam FC, BancABC na TFF, wakiwa katika picha ya pamoja na kombe la ubingwa huo, mara baada ya mkutano huo leo.
Baadhi ya viongozi wakuu wa Simba, Jamhuri, Mtibwa Sugar, Azam FC, BancABC na TFF, wakiwa katika picha ya pamoja na kombe la ubingwa huo, mara baada ya mkutano huo wa kutoa ratiba ya michuano hiyo, hatua ya nusu fainali leo.
No comments:
Post a Comment