Wanyange wakiwa wamepozi kwa picha, wakati wa mazoezi yao hivi karibuni.
Wanyange wa Miss Sinza wakipozi katika pozi la nguvu kwenye mazoezi yao |
Wanyange wa Miss Sinza wakiwa katika pozi la aina yake. |
Warembo wa Redds Miss Sinza wakimwangalia mwalimu wao, wakati walipokuwa kwenye mazoezi ya kujifua katika kambi yao hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu
WAKATI
bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) itapamba shindano la kumsaka
mrembo wa Redds Miss Sinza 2012 lillopangwa kufanyika Ijumaa kwenye
ukumbi wa Mawela Social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya
Vatican City, Kamati ya Miss Tanzania leo itatembelea warembo hao kwa lengo la ‘kuwafunda’ tayari kupanda jukwaani.
Mratibu wa kampuni ya
Calapy Entertainment, Majuto Omary alisema jana kuwa Twanga Pepeta
imeandaa zawadi kwa mashabiki wake na wale wa urembo kwa kuwapa uhondo
wa nyimbo mbili mpya ambazo zitakuwa zinasikika kwa mara ya kwanza
jukwaani.
Nyimbo
hizo ni Mapambano ya Maslahi uliotungwa na Muumin Mwinjuma, Shamba la
Twanga ambao umetungwa na Greyson Semsekwa na mmoja ambao haujapewa jina
uliotungwa na Jumanne Saidi ambaye amfunga ndoa na mnenguaji wa bendi
hiyo, Asha Sharapova.
Alisema kuwa nyimbo hizo ni zawadi kwa mashabiki wa Twanga wa Sinza na vitongoji vyake kwani bendi hiyo haijafanya shoo huko muda mrefu.
“Tunatarajia
kuwa na shoo nzuri kutoka kwa warembo na bendi ya Twanga Pepeta ambayo
mwaka huu imeshinda tuzo mbili katika tuzo za muziki Tanzania,” alisema.
Kuhusiana
na ziara ya Kampuni ya Lino International Agency, Majuto alisema kuwa
Lundenga na wenzake watafanya mazungumzo na warembo hao baada ya mazoezi
yao ya pamoja.
Alisema
kuwa ziara hiyo ni moja ya faraja kwa warembo na kamati ya Miss Sinza
kutokana na ukweli kuwa ujio wao ni wa Baraka na hitimisho la mashindano
ya vitongoji nchini.
“Miss
Sinza ndiyo inafunga pazia la mashindano ya Vitongoji (vituo) nchini,
Lundenga na wenzake wanakuja kutoa baraka zao kabla ya kuanza
pilikapilika za Redds Miss Tanzania,” alisema.
Shindano
hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti
Fashion, Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta
na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.
No comments:
Post a Comment