Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, alipopelekwa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Namala Mkopi leo, kusomewa shitaka la kutokutii amri halali ya Mahakama Kuu, iliyomtaka kuwatangazia wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari, kusitisha mgomo wao.
Rais
wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi akiwa chini ya
ulinzi wa askari Polisi na Magereza, wakati akiingia Mahakamani Kisutu leo kwa ajili ya kusomewa shitaka hilo.
Rais
wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi akiwa chini ya
ulinzi wa askari Polisi wakati akiingia Mahakamani leo.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi akiwa chini
ya ulinzi wa askari Polisi wakati akisindikizwa kuingia Mahakama ya Kisutu kwa kusomewa shitaka linalomkabili la kutotii amri halali ya Mahakama Kuu iliyomtaka kuwatangazia wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari, kusitisha mgomo wao.
Rais
wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi akiwa na mama
yake mzazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa shitaka lake hilo.
Rais
wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi (kulia)
akiongozana na baba yake mdogo, Hilary Chinendachi mara baada ya
kupoata dhama katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es
Salaam leo, aliposomewa shiataka lake hilo.
Rais
wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi akipeana mikono
na baadhi ya madaktari waliofika kujua hatma yake baada ya kufikishwa
Mahakamani kwa kosa la kukaidi amri ya Mahakama Kuu iliyomtaka kuwatangazia wanachama wa chama hicho, kupitia vyombo vya habari kusitisha
mgomo wao.
Rais
wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi akiwa na mama
yake mzazi (katikati), pamoja na baba yake mdogo, Hilary Chinendachi
mara baada ya kupatiwa dhama katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu
jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi, akizungumza jambo na Mwanasheria ambaye pia ni wakili wake, Kikondo Maulidi (kushoto), baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mahakama ya Kisutu leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk, Francis Dande)
No comments:
Post a Comment