
Bunge La Misri
Bunge la Misri limerejelea vikao vyake mapema hii leo kufuatia
agizo lililotolewa na rais mpya wa nchi hiyo Mohamed Mosri, lakini kikao hicho
kikaahirishwa baada ya muda mfupi.
Bunge hilo lilirejelea vikao vyake na kukiuka agizo lililotolewa na Baraza la
Kijeshi linalotawala, ambalo lilivunja bunge hilo kufuatia uamuzi wa mahakama ya
kikatiba.Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, mapema hii leo, Baraza hilo la Kijeshi lilisema kuwa ni sharti raia wote wa nchi hiyo waheshimu uamuzi uliotolewa na mahakama ya kikatiba.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo, anasema malumbano makali yanaendelea kutokota kati ya rais Morsi na maafisa waandamizi wa jeshi. Hata hivyo rais Morsi alijitokeza hiyo jana katika hafla rasmi ya serikali akiandamana na maafisa kadhaa waandamizi wa Baraza hilo la Kijeshi.
No comments:
Post a Comment