TANGAZO


Wednesday, July 11, 2012

Albino kupambana na Wabunge Jumamosi mjini Dodoma

Meneja wa Kinywaji cha Grand Malta, Consolata Adam akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kuhusu mechi ya kirafiki kati ya Wabunge na timu ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino  United, utakaofanyika Jumamosi mjini Dodoma na kudhaminiwa na TBL kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malta. Kushoto ni Seif Kulate, Said Ndonge na Mohamed Kindunyo.
Katibu wa timu ya Albino United, Mohamed Kindunyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu pambano lao hilo na Wabunge litakalofanyika mjini Dodoma Jumamosi, Julai 14, 2012. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment