TANGAZO


Saturday, June 16, 2012

Huduma za NHIF zawafurahisha wanavikundi vya WAMA


Ofisa anayeshughulikia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Rehani Athumani ambaye ndiye mtoa mada mkuu katika mafunzo ya akinamama wa WAMA, akifafanua jambo kwa wanavikundi zaidi ya 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), wakati wa semina ya mafunzo kwa wanavikundi hao juu ya utaratibu wa huduma zitolewazoto na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, katika ukumbi wa Mikutano wa Boma,Ilala jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanavikundi zaidi ya 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakifuatilia kwa makini mafunzo juu ya utaratibu wa huduma zitolewazoto na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,katika ukumbi wa Mikutano wa Boma,Ilala jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanavikundi hao wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliokuwa yakitolewa na mwelimishaji huyo, wakati wa semina yao, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Eugen Mikongoti akizungumza na wanavikundi zaidi ya 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati wa akifungua mafunzo kwa wanavikundi hao juu ya utaratibu wa huduma zitolewazoto na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,katika ukumbi wa Mikutano wa Boma,Ilala jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Tabu Lokoko na katikati ni Ofisa anayeshughulikia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athuman. (Picha zote na http://othmanmichuzi.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment