TANGAZO


Friday, June 15, 2012

Benki ya Posta Tanzania yaisadia Twiga Stars milioni 3

 Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi, akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa sh. milioni 3 kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake, Twiga Stars, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kusaidia maandalizi yao kutokana na kukabiliwa na michezo mbalimbali ya Kimataifa. Kulia ni Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Nasra Juma Mohamed. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (F.A), Lina Kessy akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa kukabidhiwa msaada wa sh. milioni 3 zilizotolewa na benki ya Posta Tanzania (TPB) na kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi (kulia), jijini Dar es Salaam leo.


 Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi (kulia), akimkabidhi sh. milioni 3, Nahodha wa timu ya Taifa ya Soka ya wanawake, Twiga Stars, Asha Rashid 'Mwalala', Dar es Salaam leo, ikiwa ni msaada uliotolewa na benki hiyo, kuiwezesha kufanya maandalizi ya mashindano mbalimbali ya Kimataifa. Twiga Stars kesho inajitupa uwanja wa Taifa, kuikabili Ethiopia katika kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Afrika kwa wanawake (AWC). Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (F.A), Lina Kessy na wa pili kulia ni Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Nasra Juma Mohamed.


  Nahodha wa timu ya Taifa ya Soka ya wanawake, Twiga Stars, Asha Rashid 'Mwalala', akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa sh. milioni 3, kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi (kusho), zilizotolewa na TPB, kusaidi maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya michezo mbalimbali ya kimataifa. Katikati ni Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Nasra Juma Mohamed.


 Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Nasra Juma Mohamed, akizungumza kwa ajili ya kutoa shukurani kwa TPB, kwa kuwapa msaada huo. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi, aliyekabidhi msaada huo na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (F.A), Lina Kessy.


Ofisa Masoko wa TPB, Idd Kibwana, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (F.A), Lina Kessy (wa pili kulia), Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Nasra Juma Mohamed (kushoto) na Nahodha wa timu ya Taifa ya Soka ya wanawake, Twiga Stars, Asha Rashid 'Mwalala', mara baada ya kupokea msaada huo kutoka benki hiyo jijini leo.

No comments:

Post a Comment