Baadhi ya warembo watakaochuana katika kinyang'anyiro hicho, wakiwa na Muandaaji wa kinyanganyiro hicho, Mkurugenzi wa ZUM Fashion and Entertainment, Zuwena Mustafa (kushoto), wakurahia jambo wakati wa mkutano huo jijini leo.
Mratibu wa shindano hilo, Yarson Mashaka (kulia), akizungumza katika mkutano huo, kuelezea hatua iliyofikiwa katika kuwaandaa warembo hao kimashindano kwa kinyang'anyiro hicho hadi sasa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini leo. Wa pili kulia ni Afisa Habari wa Kampuni ya ZUM Fashion and Entertainment, waandaaji wa kinyang'anyiro hicho, Sam Mshana.
Baadhi ya warembo watakaochuana katika shindano hilo, wakiwa na Muandaaji wa kinyanganyiro hicho, Mkurugenzi wa ZUM Fashion and Entertainment, Zuwena Mustafa (kushoto), wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo leo.
Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kurasini 2012, wakipozi kwa ajili ya picha mara baada ya waandaaji wa shindano hilo, Kampuni ya Zum Fashions and Entertainment, kutangaza zawadi kwa washindi wa shindano hilo, Dar es Salaam leo, litakalofanyika ukumbi wa Equator Grill, Mtoni jijini keshokutwa.
ZUM FASHION YATANGAZA ZAWADI ZA WASHINDI REDD'S MISS KURASINI 2012
Na Asha Kigundula
SHINDANO la kumsaka Redd's Miss Kurasini 2012 likitarajiwa kufanyika keshokutwa kwenye ukumbi wa Equator Grill uliopo Mtoni jijini Dar es Salaam, ambapo mrembo atakayetwaa taji hilo atazawadiwa kitita cha sh.500,000.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Zum Fashions and Entertainment, inayoandaa shindano hilo, Zuwena Mustapha, alisema kwamba maandalizi ya shindano hilo yanaendelea ambapo warembo 16 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.
Alisema mshindi wa pili ataondoka na sh. 350,000, huku mshindi wa tatu akipata sh. 250,000, wakati mshindi wa nne na wa tano kila mmoja atapata sh. 200,000 na washiriki waliosalia kila mmoja atapata sh. 200,000.
Zuwena aliongeza kuwa warembo hao wanaendelea na mazoezi katika ukumbi huo, chini ya ukufunzi wa mshindi wa taji la vipaji katika fainali za Miss Tanzania mwaka 2011, Rose Herbert.Taji la Miss Kurasini linashikiliwa na Mwajabu Juma ambaye pia anashikilia taji la Top Model la Miss Tanzania mwaka 2011.
Aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Tulekene Seth, Christina Moses, Flaviana Maeda, Farida Mrope, Edina Magige, Nzelani Juma, Anna Zakaria, Linda Deus, Angle Gasrper, Zuhura Sadiki, Mwanaisha Zuberi, Irene Sostenes, Sia Kimambo, Lilian Joseph, Asha Musa na Betty Peter.
Alisema kuwa bendi ya muziki wa dansi ya Fm Academia na Malkia wa taarab nchini, Khadija Omar Kopa wanatarajiwa kupamba fainali za shindano la Miss Kurasini mwaka 2012, zitakazofanyika keshokutwa ukumbi wa Equator Grill, uliopo Mtoni Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Miss Kurasini imedhaminiwa na Lady Pepeta, Flexip, Redd's, Pj Amusement, Dodoma Wine, Renzo Salon, Madirisha Video Production, Jambo Leo, Aucland Tours and Safaris, Clouds Fm, Father Kidevu Blog, Candy Bureau de Change, Neema Classic Wear na Giraffe Ocean View Hotel.






No comments:
Post a Comment