Mlimbwende Angel Gasper (19), mwenye elimu ya Chuo Kikuu, atakuwa ni mmoja wa warembo watakaopanda jukwaani kwa ajili ya kulisaka taji la Redd's Miss Kurasini 2012, keshokutwa jioni, Equator Grill, Mtoni Temeke, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Betty Peter (22), ni mshiriki mwenye elimu ya Chuo Kikuu, ambaye amesema kwamba taji hilo ni mali yake kwani amejitayarisha vya kutosha na pia kuyashika vyema mafunzo waliyofundihswa na walimu wao.
Blessing Kibona (22), anasoma Kidato cha Tano na ameueleza mtandao wa Blogu ya Bayana, kuwa kamwe hawezi kufanya mchezo na taji hilo kwani ndilo litakalomfanya kukata tiketi ya kushiriki kinyang'anyiro cha Redd's, Miss Tanzania 2012.
Christina Moses (19), elimu yake ni ya Chuo Kikuu, naye amesema kamwe hatofanya mchezo katika kuliwania taji hilo na kuongeza kwamba mbali ya kuvikwa taji hilo na kujinyakuliwa zawadi kabambe lakini pia usongo wake uko katika kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania ambayo tiketi yake ni pambano huo wa kitongoji cha Kuasini.
Edina Magige (19), elimu yake ni ya kidato cha nne, ameuambia mtandao wa bayana kwamba kamwe hatokubali kushindwa kirahisi, atapambana hadi mwisho na hatimaye aweze kujinyakuliwa moja ya nafasi za juu za kinyang'anyiro cha Redd's Miss Kurasini 2012.
Eliza Mkende (20), elimu yake ya kidato cha sita naye hakusita kueleza matarajio yake katika kinyang'anyiro hicho na kusema kuwa yeye nafasi yake ni kulinyakua taji hilo tu si kitu kingine.
Farida Mrope (23), elimu yake ni ya kidato cha sita. Akieleza matarajio yake, amesema kuwa ni mapambano tu, mwanzo hadi mwisho na hatimaye ni kuvishwa taji la Redd's Miss Kurasini 2012.
Flavian Maeda (22), elimu yake ni ya Chuo Kikuu. Amesema "Liwalo na liwe, hapana mchezo hapa ni kazi tu, mbele kwa mbele hadi mwisho, taji nitachukua tu, tungojane Redd's Miss Tanzaniaaaa," alimaliza.
Irene Sosthenes (20), elimu yake ni ya Chuo Kikuu. Naye hakusita kuweka bayana azma yake ya kulinyakuwa taji hilo kwa kusema maneno mafupi tu ya "ngoja utaona mwenyewe siku hiyo, mimi sisemi mengi lakini mwisho, utaona jeuri yangu", alimaliza.
Lilian Joseph (20), elimu yake ni ya kidato cha sita. Yeye pia alieleza bayana kiu yake katika kulisaka taji hilo kwa udi na uvumba hadi kulitwaa. "Nakwambia ni mimi tuuu Redd's Miss Kurasini 2012," alimaliza.
Linda Deus (20), elimu yake ya Chuo Kikuu. Anasema, "angali tabasamu tu kwanza, bado mambo mengine, utayaona kesho kutwa Equator Grill, nasema patachimbika pale hadi nilitwae taji hilo," alisema.
Linda Nancy Joseph (20), elimu yake ni ya Chuo Kikuu. Alijigamba kulitwaa taji hilo kiulaini bila kusumbuka kwani alisema kuwa mbinu na sifa zote anazo kwa taji hilo.
Sia Kimambo (19), elimu aliyonayo ni ya Chuo Kikuu na ameuambia mtandao wa blogu ya bayana kwamba kamwe hatishwi mtu, ushindi wa taji hilo ni lazima tu na kwamba kinyang'anyiro hicho kwake anakiona kwamba ni kama zoezi tu la kulitafuta taji la Redd's Miss Tanzania 2012.
Mkurugenzi wa ZUM Fashion, waandaaji wa Redd's Miss Kurasini, Zuwena Mustafa (kulia), akiwa na Mwalimu wa warembo hao, Rose Hubert (Miss Talent Tanzania 2011), wakipozi kwa picha leo asubuhi.
Kutoka kushoto warembo Angel Gasper, Irene Sosthenes na Farida Mrope, wakipozi kwa picha mara baada ya Kampuni ya ZUM Fashion kutangaza zawadi kwa washindi wa shindano hilo, litakalofanyika Ijumaa Mei 25 jioni, Equator Grill, Mtoni Temeke, jijini Dar es Salaam.
Warembo Blessing Kibona, Sia Kimambo na Flavian Maeda, wakipozi na kutoa tabasamu la nguvu wakati wa kuchukuliwa picha yao.
Warembo Edina Magige, Christina Moses na Lilian Joseph wakionesha moja ya pozi wakati wa kuchukuliwa picha.
Walimbwende Linda Nancy Joseph, Betty Peter na Linda Deus, wakiwa katika pozi la nguvu wakati wa kuchukuliwa picha.



















No comments:
Post a Comment