TANGAZO


Thursday, May 3, 2012

Waziri Ngeleja, atembelea Mamlaka ya RUBADA na kuzungumza na Wajumbe wa Bodi

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Profesa Raphael Mwalyosi, akizungumza katika utangulizi wa kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (katikati), wakati alipowatemebelea kuangalia shughuli za Mamlaka hiyo, kwenye sekta ya Nishati, inayotokana na maji kwenye bonde la mto huo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA, Aloyce Masanja. (Picha zote na Kassim Mbarouk)



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA, Aloyce Masanja, akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo na pia hazina zinazopatikana kwenye bonde la mto huo, wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kulia), kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo, jijini leo.


 Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), wakati alipofanya ziara ya kuangalia shughuli za Mamlaka hiyo kwenye Sekta ya Nishati inayotokana na nguvu ya maji (hydropower), kwenye bonde la mto huo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Mkuugenzi Mkuu wa RUBADA, Aloyce Masanja.


Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wakati alipofanya ziara ya kuangalia shughuli za Mamlaka hiyo, kwenye Sekta ya Nishati inayotokana na nguvu ya maji (hydropower), alipokuwa akizungumza nao. Katikati ni wapigapicha na waandishi wa habari, wakifuatilia ziara hiyo.



 Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), wakati alipofanya ziara ya kuangalia shughuli za Mamlaka hiyo kwenye Sekta ya Nishati inayotokana na nguvu ya maji, kwenye bonde la mto Rufiji. Wapili kulia ni Kaimu Mkuugenzi Mkuu wa RUBADA, Aloyce Masanja na Mjumbe wa bodi, Profesa Idris Mtulia.


Mmoja wa wajumbe wa bodi ya RUBADA, Dk. Aldo Lupala, akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ngeleja na kumshukuru kwa jinsi anavyoyafahamu masuala mbalimbali yanayohusiana na Mamlaka hiyo na kumsifu pia kwa ziara yake hiyo. 



Mjumbe wa bodi ya RUBADA, Profesa Idris Mtulia, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusianayo na Mamlaka hiyo, pamoja na uendelezwaji wa hazina iliyo kwenye bonde la mto Rufiji kwa Waziri Ngeleja wakati wa zaiara yake hiyo.


 Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), wakati alipofanya na mazungumzo ya kuangalia shughuli za Mamlaka hiyo kwenye Sekta ya Nishati inayotokana na nguvu ya maji kwenye bonde la mto huo.


Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya RUBADA, wakipiga picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (wa nne kushoto) pamoja na baadhi ya Maofisa kutoka Wizara hiyo, aliofuatana nao katika ziara yake hiyo leo.

No comments:

Post a Comment