Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, akiwa amebebewa juu na wanachama wa chama hicho, mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam, kumtangaza mshindi katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyokuwa ikimkabili, iliyofunguliwa na mpinzani wake, Hawa Ng'humbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mara baada ya uchaguzi huo, uliofanyika Oktoba 2010.
Wafuasi wa Chadema, wakiwa wamefurika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, kusikiliza hukumu ya Mbunge huyo.
Askari Polisi wakiwa wameweka ulinzi mkali eneo la Mahakama Kuu, Dar es Salaam, wakati wa kusomwa hukumu ya kesi hiyo leo.
Wafuasi wa CHADEMA, wakishangilia nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam leo mara baada ya hukumu iliyomhalalisha Mbunge John Mnyika kutolewa.
Msafara wa magari ya Jeshi la Polisi, ukiufuatilia na kuusindikiza msafara wa sherehe za kumsindikiza Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, wakati ukitoka Mahakama Kuu, baada ya kutolewa hukumu ya kesi ya kupinga ubunge wake leo mchana. Hapa ilikuwa katika makutano ya Barabara za Maktaba na Bibi Titi, zamani UWT.
Kijana ambaye hakujulikana jina lake akiwa amebebwa baada ya kuanguka kwenye pikipiki wakati wa msafara wa Mbunge huyo.
Mbunge wa Ubungo, Johni Mnyika (katikati mbele mwenye suti ya Chama hicho), akiwaongoza wafuasi na mashabiki wa Chama chake katika shamra shamra za kushangilia ushindi wake, Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam leo, wakielekea Jimboni kwake Ubungo jijini.
Msafara ukiwa njia panda (makutano) ya Mrogoro na Mandela (Bandari), jimboni Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari, wakichukua picha za msafara na matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye msafara wa Mbunge John Mnyika.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, akiwahutubia wananchi pamoja na wanachama wa chama chake, mara baada ya msafara uliomsindikiza kuwasili kwenye Jimbo lake la Ubungo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Philemon Solomon wa Fullshangwe)










No comments:
Post a Comment