Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la ATC, Paul Chizii (kulia), akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, mara
baada ya ndege mpya ya Shirika hilo kutua katika Uwanja wa ndege wa Mwanza mchana huu ambapo
wafanyakazi pamoja na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakitumia ndege za shirika
hilo katika kusafiri wameonekana kufurahia sana kuanza kwa safari za
shirika hilo. Katika Uwanja wa ndege wa Mwanza kutakuwa na hafla fupi ya kupongezana
kwa ajili ya kuikaribisha ndege hiyo ambapo pia keki itakatwa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa safari zake.
Abiria mbalimbali wakishuka mara baada ya ndege hiyo kuwasili jijini Mwanza mchana wa leo.
Dada Lilian wa ATC, akiwa katika pozi mara baada ya kushuka kwenye ndege hiyo leo jijini Mwanza.
Abiria wakishuka kwenye ndege hiyo mpya ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC).
Abiria wakishuka kwenye ndege jijini Mwanza, wakati ndege mpya ya Shirika la ndege Tanzania (ATC), ilipowasili ikiwa ni safari yake ya mwanzo tokea iwasili nchini mwanzoni mwa wiki. (Picha zote na John Bukuku wa Fullshangwe)






No comments:
Post a Comment