TANGAZO


Friday, May 18, 2012

Mamia wauaga mwili wa Mafisango wa Simba, Viwanja vya Sigara ni vilio tu

Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), wakilibeba jenenza lenye mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba, marehemu Patrick Mafisango, tayari kwa kutolewa heshima za mwisho leo kwenye Viwanja vya (TCC), Chang'ombe, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Dotto Mwaibale)

Msafara wa mwili wa Mafisango, ukiongozwa na Trafiki, kuingia Viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam leo.

Gari lililokuwa limeubeba mwili wa Mafisango likiingia kwenye Viwanja vya Sigara (TCC), Chang'ombe kwa ajili ya kuuaga mwili huo.
Baadhi ya watu waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mafisango, wakiwa wamejipanga tayari kuupokea kwenye Viwanja vya TCC Chang'ombe.

Mmoja wa ndugu wa karibu wa marehemu Mafisango, akilia kwa uchungu, Viwanja vya Sigara, TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.


Shabiki aliyekuwa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kuuaga mwili wa Mafisango, akilia kwa uchungu baada ya kuuaga leo asubuhi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Rwanda kwa mazishi.

Mchezaji wa Simba na Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto akilia huku akifarijiwa na baadhi ya wapenzi na mashabiki waliokwenda kuuaga mwili huo, viwanjani hapo leo.

Waombolezaji walikuwepo kwenye viwanja hivyo, wakimfariji mlinda mlango wa Simba, Juma Kaseja aliyekuwa akilia kwa uchungu.

Mmoja wa wombolezaji akiwa ameshika bango la kumuombe dua marehemu Mafisango, wakati wa kuuaga mwili wake viwanja vya TCC, Chang'ombe jijini leo asubuhi.

Mchungaji akiendesha Ibada maalumu ya kuuombea na kuaga mwili wa marehemu Mafisango, Viwanja vya Sigara.

Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesiga Selestine, akitoa salamu za klabu yake ya Yanga wakati wa kuugana mwili wa Mafisango.

Umati wa waombolezaji uliokuwepo kwenye viwanja vya Sigara, ukiwa umetulia kusubiri zamu zao kwa ajili ya kuuaga mwili wa Mafisango huku Askari Polisi wakilinda usalama, viwanjani hapo.
 
Mwanachama maarufu wa Simba, Philemon Sarungi, akimfariji Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, ambaye alishindwa kujizuia wakati akisoma risala na kuangua kilio.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah akisoma salamu za rambirambi za Shirikisho hilo, viwanjani hapo.

Mwili wa marehemu Mafisango, ukiwa kwenye jenenza lake, ukiagwa Viwanja vya Sigara, TCC Chang'ombe jijini.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mafisango.

Baadhi ya viongozi wa michezo nchini Alhaj Kipingu na Leonard Thadeo, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mchezaji huyo.

Baadhi ya wachezaji wakiwa kwenye foleni tayari kwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Patrick Mafisango.

Wananchi, wachezaji na waombolezaji mbalimbali wakiwa wamejipanga kwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mafisango.

Mwombolezaji akilia kwa uchungu kwenye viwanja vya Sigara (TCC), Chang'ombe wakti wa kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisago.

Golikipa wa Yanga, Shaaban Kado (kulia), pamoja na waombolezaji wengine wakiuombea dua mwili wa marehemu Mafisango baada ya kuuaga.
Mama shabiki wa Simba, akimwaga chozi wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisango, viwanja vya Sigara, TCC Chang'ombe.
Mchezaji wa Yanga na Taifa Stars, Nurdin Bakari, akimfariji kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto, wakati wa kuuaga mwili huo.


Sehemu ya umati wa waombolezaji waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mafisango ukiwa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa heshima zao.

No comments:

Post a Comment