Mwenyekiti wa Makampuni ya Globex Computer Services ya India, Harbhajan Singh, watengenezaji wa vifaa vya electronic, akimuonesha mmoja wa wateja waliofika kwenye banda leo, kifaa cha kutumia sola kinachotumika kuchagia simu, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana, (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Msaidizi Menja wa Mauzo wa Kampuni ya KIMMCO, Jacob Mathew wa Kuweit, akimpatia maelezo mwananchi mwenye asili ya India, aliyefika kwenye banda lao hilo kwa ajili ya kuangalia bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikioneshwa na kampuni hiyo, Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa Kompuni ya uuzaji wa spea za magari na vipuri ya Zanzibar Spear Centre, wakiwa kwenye banda lao hilo kusubiri wateja kwa ajili ya kuwapatia maelezo ya matumizi sahihi ya vipuri vyao hivyo mara baada ya kufunguliwa kwa maonesho hayo, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Oman, wakiwa kwenye banda lao, kusubiri wateja mara baada ya kufunguliwa maonesho hayo ya Biashara ya 16 ya Kimataifa, Afrika Mashariki, yanayofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.
Wafanykazi wa kampuni ya migodi kutoka India, wakisubiri maonesho hayo, kufunguliwa ili kuwapatia wananchi huduma mbali mbali jijini leo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara, Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ndibalema Mayanja, akizungumza na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, wakati alipokuwa akitafungua Maonesho ya 16 ya Kimataifa ya Biashara ya Afrika Mashariki, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo. Makampuni ya nchi za ndani na nje zaidi ya 54, yanashiriki maonesho hayo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ndibalema Mayanja, akikata utepe ili kuyafungua Maonesho ya 16 ya Kimataifa ya Biashara ya Afrika Mashariki, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo, ambapo Makampuni ya ndani na nje zaidi ya 54, yanashiriki maonesho hayo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ndibalema Mayanja, akipokea shada la maua alilokuwa akikabidhiwa na Rukhsaar Varda, mara baada ya kuyafungua Maonesho ya 16 ya Kimataifa ya Biashara ya Afrika Mashariki, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ndibalema Mayanja, akikabidhiwa kijarida cha maelezo ya Kampuni ya Kirby na Meneja Mauzo wa Kanda wa Kampuni hiyo, wakati alipokuwa akiyatembelea mabanda ya biashara mara baada ya kuyafungua maonesho hayo jijini leo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ndibalema Mayanja, akipatiwa maelezo ya Kampuni ya Kirby na Meneja Mauzo wa Kanda wa Kampuni hiyo, Murali Krishna, wakati alipokuwa akiyatembelea mabanda ya biashara mara baada ya kuyafungua maonesho hayo jijini leo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ndibalema Mayanja, akiagana na Meneja Mauzo wa Kanda wa Kampuni ya Kirby, Murali Krishna, wakati alipokuwa akiyatembelea mabanda ya biashara mara baada ya kuyafungua maonesho hayo jijini leo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ndibalema Mayanja, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuyafungua Maonesho ya 16 ya Kimataifa ya Biashara ya Afrika Mashariki, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.













No comments:
Post a Comment