Maharusi, Bw.Oltesh Eliguard Metili
na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiaga watu mbalimbali waliofika ndani ya kanisa la
Azania Front,mara baada ya kufunga ndoa takatifu, mapema leo mchana jijini
Dar.
Maharusi wakiwa na nyuso za furaha
mara baada ya kufunga ndoa na kuwa mwili mmoja mapema leo ndani ya kanisa la
Azania Front,jijini Dar.
Maharusi wakilishana kiapo cha ndoa
mbele ya umati mkubwa (haupo pichani) uliofika kanisani hapo mapema leo mchana
kuishuhudia ndoa hiyo ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu
Sylvia Nyinondi,iliyofanyika ndani ya kanisa la Azania
Front.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Askofu Dk Alex Malasusa akizibariki pete za ndoa za maharusi kabla ya
maharusi hao kuvishana.
Baadhi ya Wanakwaya kutoka mkoani
Arusha wakiimba
Umati wa watu uliofika kuishuhudia
ndoa ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi
iliyofanyika mapema leo mchana ndani ya kanisa la Azania Front,jijini
Dar.
Maharusi wakiingia ndani ya kanisa
la Azania Front mapema leo mchana,tayari kwa kufunga ndoa takatifu,pichani shoto
ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Mh Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa
wakishuhudia pia tukio hilo adhimu na la kihistoria kwa
Wanandoa.
Maharusi Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu
Sylvia Nyinondi wakiwa na wapambe wao wakielekea kanisani,tayari kwa kufunga
ndoa takatifu,mapema leo mchana. (Picha na Michuzijr
Blog)






No comments:
Post a Comment