TANGAZO


Monday, May 21, 2012

Mama Aisha Bilal, awa mgeni rasmi miaka 2 ya Tushikamane Pamoja Foundation

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Aisha Bilal, akimkabidhi zawadi ya ua mmoja wa wanachama wa Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation’,  Joha Simba, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, Me i 20, 2012. (Picha zote na Amour Nassor)


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Aisha Bilal, akimkabidhi zawadi ya ua mwanamitindo maarufu, Mustafa Hassanali, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, usiku wa kuamkia leo, Mei 20, 2012.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Aisha Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee.


Mke wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Margareth Sitta, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini usiku wa kuamkia leo.


Mchezaji wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo,  wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika Ukumbi wa Diambond Jubilee, usiku wa kuamkia leo, Mei 20, 2012.


Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, akipita jukwaani na vazi la harusi kwa mikogo,  wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation Diambond Jubilee, usiku wa kuamkia leo, Mei 20, 2012.



Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Aisha Bilal, akipozi kwa picha na Mrembo wa Utalii, Flavian Matata wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, usiku wa kuamkia leo.

No comments:

Post a Comment