TANGAZO


Monday, May 21, 2012

Zungu, Mihewa wawapiga msasa Wajumbe Kamati za Siasa za Matawi Ilala


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Suleiman Kalanje, akizungumza katika mkutano wa wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, uliofanyika ukumbi wa CCM, Boma Ilala jijini Dar es Salaam juzi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, wakiwa katika mkutano wao uliofanyika ukumbi wa CCM, Boma Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwasikiliza viongozi Mkoa na Wilaya walipokuwa wakizungumza nao kuhusiana na chaguzi za chama chao zinazoendeleo nchini hivi sasa.


Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza na wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, wakati wa mkutano wa kuwapiga msasa kwa ajili ya chaguzi za Chama, zinzoendelea nchini hivi sasa. Mkutano huo, uliofanyika ukumbi wa CCM, Boma Ilala jijini Dar es Salaam juzi.


Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza na wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, katika  mkutano wa kuwapiga msasa wajumbe hao kwa chaguzi za Chama, zinzoendelea nchini hivi sasa. 


 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akisisitiza jambo katika mkutano huo wa wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, uliofanyika ukumbi wa CCM, Boma Ilala jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Katibu wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Ilala, Suleiman Kalanje.


Wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, wilayani Ilala, wakiwa katika mkutano wao uliofanyika ukumbi wa CCM, Boma jijini Dar es Salaam, wakiwasikiliza viongozi wao wa Mkoa na Wilaya, walipokuwa wakizungumza nao kuhusiana na chaguzi za chama chao zinazoendeleo nchini hivi sasa.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa, akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, Wilaya ya Ilala jijini juzi, wakati alipokuwa akiwapiga msasa kwa ajili ya chaguzi za Chama chao zinzoendelea nchini hivi sasa. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' na Diwani wa Viti Maalum, Tumike Malilo. 


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa, akizungumza na wajumbe wa Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, wilayani Ilala, jijini juzi, wakati alipokuwa akiwapiga msasa kwa ajili ya chaguzi za Chama.


 Baadhi ya wazee wa CCM, waliokuwepo kwenye Kamati za Siasa za Matawi ya Chama hicho, wilayani Ilala, wakiwasikiliza viongozi wao wa Mkoa na Wilaya wakati walipokuwa wakizungumza nao kuhusiana na chaguzi za chama chao zinazoendeleo nchini hivi sasa.

No comments:

Post a Comment