TANGAZO


Monday, May 21, 2012

Airtel yazindua SUPA 5, Coco Beach

Mmoja wa wasanii wa kundi maarufu nchini la Tip Top Connection, lenye makazi yake Manzese jijini Dare es Salaam, ajulikanae kwa jina la Dogo Janja, akiimba  katika jukwaa la Airtel SUPA 5, ambapo Airtel ilizindua huduma muhimu ya Airtel, itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma ya facebook bure, kutuma sms 200 bure, mara wanapotuma sms 10 tu kwa sh 30Tsh, kuchagua namba tatu za kuongea nazo kwa nusu shilingi tu siku nzima, kuongea kwa robo shilingi usiku kucha pamoja na kufurahia internet ya bure nyakati za usiku.


Mdau Alex Msama wa Msama Promotion, akitete jambo na mdau mwenzake wakati wa uzinduzi wa SUPA 5 ya Airtel, Coco Beach, Dar es Salaam leo.


Umati wa watu wakishangilia burudani kali toka kwa wasanii wakali wa muziki wa dansi na bongo flava wakati wakitumbuiza katika fukwe za Coco Beach, jijini Dar es Salaam wakati Airtel ilipozindua huduma mpya ya SUPA 5.


Mzee wa Kibega toka kundi la Mashujaa, Raisi kijana Charles Baba akionyesha manjojo yake ya jinsi ya kumiliki jukwaa kwa kucheza sebene kali kwa staili yao ya kibega katika fukwe za Coco Beach, Dar es Salaam leo, ambapo bendi hiyo pia ilitumbuiza wakati Airtel ilipozindua huduma yao mpya ya SUPA 5 Airtel, itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma ya facebook bure, kutuma sms 200 bure, mara wanapotuma sms 10 tu kwa sh. 30, kuchagua namba tatu za kuongea nazo kwa nusu shilingi tu siku nzima, kuongea kwa robo shilingi usiku kucha pamoja na kufurahia internet ya bure nyakati za usiku.


Msanii wa kizazi kipya Mwasiti, akionyesha umahiri wake kwa mashabiki waliojitokeza katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es salaam leo, wakati ambapo kampuni ya simu za mkononi Airtel ilipofanya tamasha maalum kwa ajili ya uzinduzi wa huduma yao mpya ya SUPA 5.

No comments:

Post a Comment