Rais wa Baraza la Chuo Kikuu cha St. Joseph (SJCET) Mbezi, Thomson Xavier, akitoa maelezo kuhusu Chuo hicho pamoja na kozi zinazofundishwa Chuoni hapo kabla ya Mweneyekiti wa Baraza la Chuo, Mhandisi Steven Mlote, kuzungumza kuhusu kuanzishwa kwa masomo ya Uhandisi kwa ngazi ya Stashahada za Ufundi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kuanzia mwaka 2011.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mhandisi Steven Mlote, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo, kuhusu kuanzishwa kwa masomo ya Uhandisi kwa ngazi ya Stashahada za Ufundi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kuanzia mwaka 2011. Kulia ni Rais wa Baraza la Chuo Kikuu cha St. Joseph (SJCET) Mbezi, Thomson Xavier na kushoto ni Menyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kibamba, Luguruni kilipo chuo hicho, Siraju Yussuf.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mhandisi Steven Mlote, akizungumza kwenye mkutano huo, hotelini hapo leo asubuhi. Katikati ni Rais wa Baraza la Chuo hicho, Thomson Xavier.
Waandishi wakisiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa Chuo hicho kwenye mkutano huo leo asubuhi, hotelini hapo.
Rais wa Baraza la Chuo Kikuu cha St. Joseph (SJCET) Mbezi, Thomson Xavier (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mhandisi Steven Mlote wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mhandisi Steven Mlote, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati walipotaka kujua masuala mbalimbali yahusianayo na upatikanaji wa wanafunzi hao kwa ajili ya kozi hizo. Katikati ni Menyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kibamba, Luguruni kilipo chuo hicho, Siraju Yussuf na Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala na Uhasibu, Sister Fatima Mary Arulandu.
Rais wa Baraza la Chuo Kikuu cha St. Joseph (SJCET) Mbezi, Thomson Xavier, akifafanua jambo wakati uongozi wa Chuo hicho, ulipokuwa ukizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuanzishwa kwa masomo ya uhandisi kwa ngazi ya Stashahada za Ufundi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kuanzia mwaka 2011. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Steven Mlote na Menyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kibamba, Luguruni kilipo chuo hicho, Siraju Yussuf.(Picha na Kassim Mbarouk)
No comments:
Post a Comment