Golikipa wa Zambia, Kennedy Mweene, akiokoa penalti ya Gervinho wakati wa mchezo wa fainali ya mashindano ya Afrika (AFCON), leo usiku mjini Libreville, Gabon.
Kennedy Akiokoa penalti ya Kolo Toure, wakati wa kupigiana penalt kwenye mchezo huo.
Stoppila Sunzu, akishangilia baada ya kufunga penalti yake ya mwisho katika mchezo huo.
Wachezaji wa Ivory Coast, wakiwa na majonzi baada ya kupoteza mchezo huo kwa njia ya kupigiana penalti. Zambia ilishinda 8-7.
Wachezaji wa Zambia wakimpongeza Stoppila Sunzu, baada ya kufanikiwa kufunga penalti yake ya mwisho, iliyowapatia ushindi dhidi ya Ivory Coast leo usiku na kukabidhiwa kombe la Ubingwa wa Afrika.
Wachezaji wa Zambia wakishukuru kwa Mungu, baada ya kufanikiwa kuwafunga wapinzani wao katika Fainal ya AFCON, Ivory Coast penalti 8-7.
Wachezaji wa Zambia wakikimbia kwa furaha baada ya Stoppila Sunzu kuifungia timu yake ya Chipolopolo penalti ya mwisho ya fainali hiyo dhidi ya Ivory Coast, leo usiku.
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, akimpoza Garvinho, wakati wa kupewa medali zao za fedha.
Yaya Toure, akipozwa na Rais wa Ivory Coast, Alassane Outtara, wakati wa kupewa medali zao za fedha.
Nahodha wa Zambia, Chris Katongo, akilinyanyua juu kombe la Ubingwa wa mashindano ya AFCON, mara baada ya kuishinda Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti 8-7, leo usiku.
Nahodha wa Zambia, Chris Katongo, akilibusu kombe la ubingwa wa AFCON, mara baada ya kukabidhiwa leo usiku.
Wachezaji wa Zambia wakifurahi, wakiwa na kombe la Ubingwa wa mashindano ya Afrika (AFCON), mara baada ya kuishinda Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti 8-7, leo usiku.
No comments:
Post a Comment