TANGAZO


Monday, February 20, 2012

Tume ya Utumishi ya Bunge la Uganda yazuru Ofisi za Bunge Dar es Salaam


Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda, Dk. Chriss Buryomunzi (katikati shati jeupe), akifafanua jambo kwa wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania (hawapo pichani), wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa maswala mbalimbali katika utawala wa Bunge, Dar es Salaam leo. Wa kwanza kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Mhe. Emmanuel Lumula Dombo(Mb), akifuatiwa na Mhe, Okupa Elija (Mb), Mhe. Dk. Chriss Buryomunzi na Dintu Jalia Lukumu Ngonzi. (Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge)


 Naibu Spika, Job Ndugai, akiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Wabunge wanaounda Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda, ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.  Ujumbe huo umewasili nchini jana, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania katika maswala mbalimbali.  (Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge)




 Naibu Spika, Job Ndugai, akiwa katika mazungumzo na ujumbe huo. Kutoka kulia kwake ni kiongozi wa msafara huo, Emmanuel Lumula Dombo, Okupa Elija,  Dk. Chriss Buryomunzi na Dintu Jalia Lukumu Ngonzi. (Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge)

No comments:

Post a Comment