TANGAZO


Monday, February 20, 2012

Rais Kikwete, azindua zoezi la Serikali kuwawesha wananchi mifugo


Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Wilaya Longido muda mfupi baada ya kuwasili wilayani hapo, ambapo aliongoza shughuli ya kutoa msaada wa ng’ombe zaidi ya 25,000 na mbuzi zaidi ya 15,000 kwa wakazi wa wilaya za Longido, Ngorongoro na Monduli, ambao mifugo yao yote iliangamia wakati wa kiangazi kikali. (Picha na Freddy Maro)

 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Wilaya Longido katika hafla hiyo jana.




 Wananchi hao, wakiwania kumpa mkono Rais Kikwete, wakati wa hafla hiyo, kabla ya kuongoza zoezi la kugawa mifugo kwa wakazi hao.


 Mwanafunzi Godlisten Ole Olais, anayesoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Longido, akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili katika viwanja vya sekondari hiyo, kuongoza uzinduzi wa wa mradi wa serikali wa uwezeshaji mifugo (seed stock), kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na 2009-2010, zilizofanyika wilayani Longido  jana.




 Mmoja wa viongozi wa kabila la Kimasai (Laigwenani), akimpa Rais Kikwete mkuki, wakati waliomkabidhi silaha za jadi za utawala, wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.




 Mmoja wa viongozi wa kabila la Kimasai (Laigwenani), akimpa Rais Kikwete zana za kijadi za uongozi, mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.


 Mmoja wa Wazee wa Kimasai akimuombea dua, Rais Jakaya Kikwete walayani Longido Jumapili.




 Mzee wa Kimasai, mkazi wa Longido, akimshukuru na kumuombea dua njema, Rais Kikwete, baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano na mbuzi watano wilayani Longido jana. Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji walipoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za Longido, Ngorongoro naMonduli.

 Morani wa Kimasai wakicheza ngoma maalumu wakati wa hafla hiyo.





Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia wananchi wa Longido wakati wa hafla ya kugawa ng’ombe zaidi ya 25,000 na mbuzi zaidi ya 15,000 kwa kaya zilizoathirika kwa ukame wilayani Longido jana.

No comments:

Post a Comment