Klabu ya soka ya Rangers, imethibitisha kwamba imewasilisha ombi lake kisheria mahakamani ikiwa na nia ya kupata watu watakaosimamia shughuli za klabu huku ikijitayarisha kutangaza kufilisika.
Klabu kimetangaza kwamba kitaendelea na shughuli zake kama kawaida, hadi kitakapotangaza uamuzi wa mwisho kama kitaendelea na hatua hiyo.
Rangers sasa ina siku 10 kufanya uamuzi.
Hayo yakiendelea, klabu kimetangaza kwamba mashabiki wenye tiketi za msimu mzima, na vile vile wenye hisa, wasiwe na wasiwasi wowote.
Hatua hiyo imechukuliwa huku Rangers ikisubiri uamuzi kuhusiana na ubishi juu ya ushuru, pamoja na faini mbalimbali, jumla ya deni ikiwa ni pauni milioni 49.
Kupitia taarifa, klabu kimeelezea kwamba ikiwa uamuzi huo utaamuliwa kwa idara ya forodha kushinda kesi, basi itamaanisha malumbikizo ya deni hilo na faini huenda yakazidi hata pauni milioni 50, na klabu hakitakuwa na uwezo wa kulilipa deni hilo.
Tajiiri anayemiliki klabu, Craig Whyte, alinukuliwa baadaye akisema deni hili huenda likazidi na kufikia pauni milioni 75.
Whyte, ambaye alinunua klabu kutoka kwa Sir David Murray mwaka jana, alisema suala la klabu kupata usimamizi mpya ni jambo la kufikiriwa iwapo klabu kitashindwa katika kesi hiyo kuhusiana na ushuru.
No comments:
Post a Comment