Rais wa Ujerumani Christian Wulff, ametangaza kujiuzulu kwake baada ya wendesha mashtaka kutaka aondolewe kinga ya kushtakiwa.
Bwana Wulff, ambaye ni mshirika wa chansela Angela Merkel, anakumbwa na kashfa kuhusu mkopo wa kununua nyumba aliopokea wakati akiwa waziri mkuu wa ufalme mdogo nchini humo.Bi Merkel alifutilia mbali ziara yake nchini Italia mnamo Ijumaa ili kuweza kukabiliana na kashfa hiyo,suluhisha kashfa na kuelezea kuwa anajuta kujiuzulu kwa bwana Wulff.
Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeelezea kuwa kashfa hiyo ndio ya kwanza ya aina yake tangun enzi ya vita nchini humo.
Bi Merkel alipambana vilivyo kuhakikisha kuwa bwana Wulff,anaunga mkono chama chake cha Christian Democrat party (CDU),kama rais wadhifa alioushikilia kwa chini ya miaka miwili.
No comments:
Post a Comment