TANGAZO


Friday, February 24, 2012

Raia zaidi watoroka vita Mali


Wakimbizi wa ndani nchini Mali
Wakimbizi wa ndani nchini Mali
Umoja wa mataifa umesema kuwa idadi ya watu wanaokimbia maeneo ya Kaskazini mwa taifa la Mali sasa imeongezeka na kufikia watu 20,000.
Takriba watu nusu milioni wamekimbilia mataifa jirani baada ya kundi jipya la waasi wa Tuareg kuanzisha mashambulio dhidi ya vikosi vya serikali wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa umoja wa mataifa takriban watu 1000 wanavuka mpaka wa Mali na kuingia katika mataifa jirani kila siku.
Hii inafanya idadi ya watu waliolazimika kuishi maisha ya ukimbizi nchini mwao na wale wanaokimbilia mataifa jirani kufikia takriban watu 125,000.
Raia hao wanatoroka mapigano kati ya vikosi vya seriki na kundi la waasi wa Tuareg, MNLA, ambao wanataka eneo la Kaskazini kujitenga na Mali.
Wakimbizi wa ndani nchini Mali
Wakimbizi wa ndani nchini Mali
Wapiganaji hao wa Tuareg walioshiriki vita vya kumlinda kanali Muamar Gaddafi wakati wa vita vya Libya, walirejea nchini Mali, wakiwa wamejihami kwa silaha nzito nzito na kuanzisha mashambulio dhidi ya miji ya Kaskazini na vituo vya kijeshi baada ya kujiunga na kundi moja la waasi.
Kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu zaidi ya watu 20 wameuwawa tangu mgogoro huo uanze lakini hadi kufikia sasa imekuwa vigumu kupata taarifa huru kuhusu hali ya mambo.
Shirika la Amnesty International, limetoa wito kwa vikosi vya serikali kukomesha mashambulizi ya bomu dhidi ya raia baada ya helikopta za kivita kurusha makombora kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani kwa ndani Kaskazini mwa taifa hilo siku ya Jumatano.
Serikali ya Mali imewashutumu waasi hao kwa kujiunga na mrengo wa Afrika ya Kaskazini wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

No comments:

Post a Comment