TANGAZO


Tuesday, February 28, 2012

Mwenyekiti Mrema, alonga na waandishi jijini Dar

 Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, asubuhi kuhusu walivyojiandaa kwa uchaguzi wa Arumeru na pia kutokukubaliana na baadhi ya Wabunge kuhusu kutaka kujiuzulu kutokana na posho ndogo wanazolipwa. Kushoto ni Katibu Mkuu Taifa, Jeremiah Mchanjala na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Utawala Nancy Mrikaria. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu matayarisho ya uchaguzi wa Arumeru na suala la kutokukubaliana na baadhi ya Wabunge kutaka kujiuzulu kutokana na posho ndogo wanazozipata.


 Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema akiwaonesha waandishi wa habari, vyeti vyake vya Shahadi ya juu ya Sayansi ya Uongozi wa Siasa, alivyovipata kutoka nchi Afrika ya Kusini baada ya kuhitimu kwenye Vyuo vya nchi hiyo, akivionesha kutokana na wale wanaotaka kujua elimu aliyonayo Mwenyekiti huyo, wakati wa mkutano huo, Dar es Salaam leo, Februari 28, 2012. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Utawala Nancy Mrikaria.

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema akiwaonesha waandishi wa habari, vyeti vyake mbalimbali vya Shahadi ya juu,  alivyovipata kutoka nchi Afrika ya Kusini baada ya kuhitimu kwenye Vyuo vya nchi hiyo. Kulia ni  Naibu Katibu Mkuu Utawala Nancy Mrikaria.

No comments:

Post a Comment