TANGAZO


Wednesday, February 22, 2012

Mwakilishi mpya wa Uchumi wa China nchini amtembelea Waziri Nagu

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji,  Dk. Mary Nagu, akisalimiana na aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania, Zhao Zhongqiu, leo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam. Zhongqiu alimtembelea Waziri huyo, kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)




 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu akimsikiliza aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini, Zhao Zhongqiu, alipokwenda ofisini kwake kumuaga . 




 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu akisalimiana na Mwakilishi  Mkuu mpya wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini,  Lin Zhiyong leo, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, alipokwenda kujitambulisha kwake. Kulia ni Zhao Zhongqiu, aliyemaliza  muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.




 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu, akizungumza na ujumbe wa wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania, kuhusu masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na China. 




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu, akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi hao, mara baada ya kuwa na mazungumzo nao.


No comments:

Post a Comment