TANGAZO


Wednesday, February 22, 2012

Dk. Bilal azindua dahalia la Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Beach wilayani Nkasi

Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi jengo la dahalia la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korongwe Beach, iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.  (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifunua pazia ili kuzindua rasmi jengo la dahalia la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.  (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

  Makamu wa Rais,  Dk. Mohammed Gharib Bilal, akinawa maji ya kisima cha pampu yanayovunwa kwa mvua, kilichojengwa katika kijiji cha Mwamapuli, wakati alipokuwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi juzi.


 Makamu wa Rais,  Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu, nje ya  jengo la dahalia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach,  iliyopo Wilaya ya Nkasi baada ya kuzindua dahalia hilo. Nyuma yake ni  mkewe Mama Asha Bilal na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mkazi wa kijiji cha Mwamapuli, Yacoub Jilala, ambaye ni mlemavu, baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho, alipofika kuzindua jengo la Ghala la mazao, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi, juzi Februari 20, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


Makamu wa Rais,  Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Korongwe kwa ajili ya kuwahutubia wananchi, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi jana Februari 21, 2012.

No comments:

Post a Comment