TANGAZO


Wednesday, February 22, 2012

Ibada ya Siku ya Majivu yafanyika Makanisani

 Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, akiwapaka majivu waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa funga ya siku arobaini (Kwaresma), wakati wa Ibada ya Majivu iliyofanyika kanisani hapo leo, Dar es Salam. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, akiwapaka majivu waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa funga ya siku arobaini (Kwaresma), wakati wa Ibada hiyo,  kanisani hapo.


 Sister Yuda Thadei, akiwapaka majivu waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph, wakati wa Ibada maalum ya Siku ya Majivu, iliyofanyika Kanisani hapo, Dar es Salaam leo.. (Picha na Kassim Mbarouk)


Baadhi ya  waumini wa Kanisa hilo, wakiwa nje ya Kanisa wakati wa Ibada hiyo, kanisani hapo.
 Baadhi ya waumini wa Kanisa hilo, wakiwa wamekaa, wakisikiliza mahubiri mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Maaskofu na Mapandre, ndani ya Kanisa hilo, wakati wa Ibada hiyo, kanisani hapo.




No comments:

Post a Comment