Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Mr II, wakati alipokuwa Uyole, kuweka jiwe la msingi katika jengo la SACCOS-UWAMU, lililopo Mbeya mjini, katika ziara yake mkoani humo jana. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo na kuangalia moja kati ya mizinga ya nyuki kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuhusu utengenezwaji wa mizinga hiyo, ya kisasa na ya gharama nafuu, wakati alipofika kutembelea kituo cha kuahiria mifugo cha Simambwe, kilichopo Wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwa katika ziara yake ya mkoni humo jana Februari 25, 2012. Kulia ni mke wake, mama Asha Bilal. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akiufunua moja ya mizinga ya kufugia nyuki kwa ajili ya kumuonesha Makamu wa Rais, wakati alipotembelea kituo cha kuahiria mifugo cha Simambwe, kilichopo Wilaya ya Mbeya Vijijini jana.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mzinga wa nyuki, Salome Zumba, mmoja kati ya wafugaji wa kikundi cha akinamama na vijana cha kijiji cha Ijewe, wakati wa ziara yake hiyo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono, ili kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Simambwe, wakati alipowasili kijijini hapo, kutembelea kituo cha kuahiria mifugo na kukabidhi mizinga ya nyuki kwa badhi ya wafugaji, akiwa katika ziara yake mkoani Mbeya jana. |
No comments:
Post a Comment