TANGAZO


Saturday, February 25, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal, aaga Katavi na Rukwa kwa kuzindua kampeni ya Ngara Sumbawanga

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa viongozi wa Kampuni za kufanya usafi katika mitaa ya mjini Sumbawanga, wakati akizindua kampeni ya Sumbawanga Ng’ara  kwa ajili ya kudumisha usafi wa mazingira, ikiwa ni siku yake ya mwisho ya ziara yake katika mkoa wa Katavi na Rukwa jana, Februari 24, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)



 Mama Asha Bilal, akionyesha mfano kwa kufagia wakati akimkabidhi mmoja wa kinamama wanaofanya usafi wa mazingira katika mitaa ya mjini Sumbawanga, jana Februari 24, 2012, wakati Makamu wa Rais alipokuwa akizindua kampeni ya Sumbawanga Ng’ara yenye lengo la kudumisha usafi wa mazingira wa maeneo hayo.


 Makamu wa Rais,  Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampeni ya Sumbawanga Ng’ara yenye lengo la kudumisha usafi wa mazingira mjini Sumbawanga. Kulia kwake ni mkewe mama Asha Bilal na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya.


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na mama Asha Bilal (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya, mbele ya Sanamu la Sumbawanga Ng’ara baada ya kuzindua kampeni hiyo jana Februari 24, 2012.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mama Asha Bilal (kushoto kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya (kulia) na baadhi ya viongozi wa mji wa Sumbawanga, mbele ya Sanamu la Sumbawanga Ng’ara baada ya kuzindua kampeni hiyo jana Februari 24, 2012.

No comments:

Post a Comment