TANGAZO


Saturday, February 25, 2012

Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, yakutana Arusha

 Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, akimkaribisha Spika wa Bunge la Rwanda, Rose Mukantabana, Mjini Arusha jana, mara alipofika nchini, kuhudhuria Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola  kanda ya Afrika (CPA Africa), unaofanyika mjini Arusha tarehe 24, Februari, 2012. Rose Mukandabana ni Rais wa Chama hicho kwa Kanda ya Afrika. (Picha na Owen Mwandumbya)




 Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai akijadili jambo na Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Mninwa Mahalangu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika, alipofika nchini kuhudhuria Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola  kanda ya Afrika (CPA Africa) unaofanyika mjini Arusha tarehe 25 Februari, 2012. 




 Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Mninwa Mahalangu (katikati), ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika, akiongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Chama hicho walipokutana mjini humo. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Rwanda, Rose Mukantabana, ambaye pia ni Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika.





Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola  kanda ya Afrika (CPA Africa), wakiwa katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Chama hicho, mjini Arusha februari, leo 25, 2012.


 Wajumbe wa Sekretariati ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola  Kanda ya Afrika (CPA Africa), wakiwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya chama hicho kilichofanyika mjini Arusha Februari, 25, 2012. 





 Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Mninwa Mahalangu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji CPA Afrika akiongoza kikao cha kamati tendaji ya chama hicho walipokutana mjini Arusha leo 25 Februari, 2012. Kushoto ni Spika wa Bunge la Rwanda Rose Mukantabana, ambaye pia ni Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika.



Katibu wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola  kanda ya Afrika (CPA Africa), Dk. Thomas Kashililah ambaye pia ni katibu wa Bunge la Tanzania akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Mninwa Mahalangu (Kulia),  wakati wa kikao cha kamati ya Uongozi ya chama hicho, jijini Arusha leo.

No comments:

Post a Comment