Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe ili kulizindua Soko la Tunduma, lililofanyiwa ukarabati baada ya kuungua kwa moto mwaka jana, wakati wa mwanzo wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya jana, Februari 24, 2012. Kushoto ni mkewe, mama Asha Bilal, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na (kulia kwake) ni Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye eneo la Soko la Tunduma kwa ajili ya kuzindua soko hilo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kufuatia moto ulioliteketeza mwaka jana. Anayefuatana naye mbele yake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Tunduma wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua Soko lao, liliokarabatiwa upya baada ya kuungua kwa moto.
No comments:
Post a Comment