Watu waliokua na silaha wamevamia jela moja iliyo Jimbo la kati nchini Nigeria na kuwaachilia wafungwa 199. Afisa mmoja wa usalama ameuawa katika shambulio hilo. Haijabainika ni nani aliyehusika na tukio hilo lililotokea katika Wilaya ya Kogi siku ya jumatano.

Ghasia Nigeria
Ghasia Nigeria

Silaha kali na bomu zilitumiwa na idadi kubwa ya washambuliaji katika shambulio la dakika 30 kwenye gereza la Kogi Jimbo lililo kusini mwa mji mkuu wa nchi wa Abuja.

Silaha kali zilitumiwa
Silaha kali zilitumiwa

Mlinzi wa magereza aliuawa mlangoni kabla ufunguliwe kwa nguvu. Hadi sasa hakuna aliyedai kuhusika na shambulio ingawa mwezi uliopita kundi lenye msimamo mkali wa Kiislamu la Boko Haram liliwaachilia wafuasi wao waliokua wakishikiliwa kufuatia milipuko ya mjini Kano ikikumbukwa kua mnamo mwaka 2010 shambulio kama hilo lilifanywa katika gereza la mkoa wa Bauchi ambako wafungwa 700 waliachiliwa.
Msemaji wa gereza huko Kogi amekanusha kua ni kundi la Boko Harm lililohusika na shambulio la hivi sasa. Amesema kua wengi wa wafungwa walioachiliwa walikua wakisubiri kesi zao lakini hakuweza kuthibitisha tuhuma zinazowakabili, kama ni za kiigaidi au ujambazi.