Wakuu nchini Yemen wanasema kua kiongozi mmoja wa mtandao wa Al Qaeda ameuawa katika kilichoelezewa kama tafauti za kifamilia. Haya yametokea katika mkoa wa kusini mwa nchi ambako wapiganaji wanaodhaniwa kua na uhusiano na al-Qaeda wametumia fursa ya vurugu za mwaka jana kujiimarisha.
Maelezo ya mauwaji kama haya kutoka duru rasmi na za kikabila yanatosha kufahamisha mengi kuhusu jinsi Yemen ilivyogawanywa kwa misingi ya matabaka na ukabila.
Tarek al-Dahab inafahamishwa kua alikua kiongozi wa al-Qaeda, aliyeongoza mashambulio ya hivi karibuni ya wakereketwa katika miji ya kusini kufaidi kutokana na vurugu zilizokua zikiendelea huko.
Suala jingine muhimu kuhusiana na kiongozi huyu ni kua alikua shemeji wake Anwar al-Awlaki,mzaliwa wa Marekani mwenye msimamo wa imani kali aliyewekwa kwenye orodha ya Marekani ya watu wanaotakiwa kuuawa na mwaka uliopita aliuawa katika shambulio la ndege inayopaa bila rubani.
Imearifiwa kua Tarek aliuawa na kakake wa kambo, Hizam, katika kile kilichotajwa kua ubishi juu ya mapato ya kikabila. Baada ya mzozo Hizam na wafuasi wake walizingirwa ndani ya nyumba walimokimbilia na wafuasi wa Tarek.
Watu 16 akiwemo Hizam, waliuawa katika mapigano yaliyofuata. Kila siku kuna habari za mapigano huko kusini mwa nchi yanayohusisha wakereketwa wa Kiislamu.
Wakereketwa hawa bado wanadhibiti mji muhimu wa Zinjibar, waliouteka katika mazingira ya kutatanisha mwezi Novemba.
Haya ni sehemu ya vigezo vinavyoikabili serikali ya mseto iliyoteuliwa baada ya Rais Saleh hatimaye kukubali kujiuzulu mwaka jana.
Uchaguzi wa Rais uliopangwa ili kukomesha enzi ya miaka 30 ya utawala wa Rais Saleh unatazamiwa siku ya jumanne ijayo.
Kuna mgombea mmoja, ambaye ni Naibu makamu wa Rais, Abdrabbu Mansour Hadi ambaye picha yake ilianza kitambo kuwekwa mahala pa Rais wa zamani.
Ushahidi zaidi ya wa hali mbovu ya usalama ni ukosefu wa utulivu mwandishi wa BBC nchini Yemen alishambuliwa na watu wenye silaha siku ya jumatano, ambao BBC ina amini kua wafuasi wa Bw.Saleh. Shirika la utangazaji la BBC limewasihi wakuu wa Yemen wahakikishe kua wandishi habari wanaendesha kazi zao bila kunyanyaswa.
No comments:
Post a Comment