TANGAZO


Thursday, February 9, 2012

Kazi afanye mume, mshahara kupewa mke

Maafisa katika jimbo la Gorontalo nchini Indonesia wamepata njia mpya ya kuhakikisha wake wa wafanyakazi wa serikali wanapata mgao wa kutosha wa mshahara wa waume zao.
Mshahara
Mshahara sasa kwenda kwa mke



Mpango huo ni kuweka fedha za mishahara katika akaunti za benki za wake wa wafanyakazi wa serikali. Mpango huo unatazamiwa kuanza mwezi Machi na unatarajiwa kuweka familia pamoja, kutokana na kongezeka kwa vitendo vya wanaume kutumia fedha za ziada kwa wanawake wa nje.Ni mpango rahisi lakini wa aina yake. Kuanzia mwezi Machi, kila mwanaume aliye na mke na anayefanya kazi katika serikali katika jimbo la Gorontalo atashuhudia mshahara wake ukiingia kwanza katika akaunti yake na mara moja fedha hizo kuhamishwa kwenye akaunti ya mke wake.
Hatua hiyo ni ya kuzuia matumizi "mabaya" ya fedha. Maafisa wanasema wamepokea malalamiko mengi mwezi uliopita kutoka kwa wake wa wafanyakazi wa serikali, ambao wanasema hwapati fedha za kutosha kutoka kwa waume zao kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Msemaji wa jimbo la Gorontalo Rudy Iriawan amesema kanuni hiyo mpya ina lengo la kulinda familia zisimeguke. "Tuna wasiwasi kwa kuwa mwanaume ndio anadhibiti fedha za familia.
Na tunataka kuhakikisha mishahara ya wafanyakazi wa serikali inatumika kujenga familia na sio kwa ajili ya mambo mengine hasa wanawake wa nje".
Hata hivyo maafisa hao pia wameonya kuwa wake wa wafanyakazi hao wa serikali wasitumie fedha kujinunulia vitu vya kifahari.
Wametakiwa kuzingatia hatua hiyo kama kazi, zimesema mamlaka, katika kutazama fedha za familia za nyumba zao.

No comments:

Post a Comment