Mahakama ya Ulaya kuhusu haki za binadamu imetoa uamuzi wake kuwa Italia ilivunja haki za binadamu kwa wahamiaji wa Eritrea na Somalia kwa kuwarudisha tena Libya.
Waeritrea 13 na Wasomali 11 walikuwa miongoni mwa kundi la watu 200 walioondoka Libya kwa kutumia boti tatu mwaka 2009. Wawili kati ya 24 walikufa.
Mwaka jana Italia ilisitisha makubaliano ya mwaka 2008 na Libya wa kuwarudisha wahamiaji nyumbani.Mahakama ilamuru Italia imlipe kila mmoja wa wahamiaji hao kwenye kesi Euro 15,000 (£13,000; $20,000).
Kitengo cha mahakama (Grand Chamber judgment) katika kesi ya Hirsi Jamaa na wengine dhidi ya Italia kilikuta walalamikaji kuwa wamekwekwa kwenye hatari ya kutotendewa haki nchini Libya na kurejeshwa Somalia au Eritrea.
Hatua hiyo ni ukiukwaji wa kifungu cha tatu cha makubaliano Ulaya kuhusu haki za binadamu kinachozuia uhalifu wa kibinadamu ua kuwawapa haki yao.
Kulikuwa pia na ukiukwaji wa wa kifungu cha Nne kinachozuia urejeshwaji wa pamoja, kwa mujibu wa makubalino ya hukumu ya majaji.
Hukumu ya Mahakama ya Juu ni ya mwisho ikimaanisha kuwa kisheria imeifunga Italia.
Mahakama ilisema kuwa mwaka 2009 Italia ilifanya operesheni tisa baharini kuzizuia boti za wahamiaji, kulingana na makubaliaono yaliyotiwa saini na waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi na kiongozi wa Libya wakati huo marehemu Kanali Muammar Gaddafi.
Februari 26 mwaka jana Italia ilitangaza kusitisha makubaliano yake baada ya machafuko ya Libya.
No comments:
Post a Comment