Walipuaji wameshambulia wafanyakazi katika ubalozi wa Israel nchini India na Georgia, maafisa wanasema, huku Israel ikiituhumu Iran kwa kuendesha mashambulio hayo.
Mlipuko mjini Delhi umejeruhi afisa mmoja wa ubalozi na watu wengine watatu.
Watu walioshuhudia wamekiambia kituo kimoja cha TV kuwa watu wawili wakiwa kwenye pikipiki walitega bomu ndani ya gari, liliposimama kwenye taa za barabarani.
Bomu chini ya gari la ubalozi mjini Tbilisi lilipatikana na kuteguliwa.
Kiongozi wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Iran inahusika na matukio hayo mawili.