Waziri wa mashauria nchi za nje wa Uingereza, William Hague, ameonya kuwa azma ya Iran ya kuwa na silaha za nuklia, itaitumbukiza Mashariki ya Kati katika vita baridi vipya.
Na hiyo itasababisha duru ya mashindano ya nuklia makubwa kabisa tangu silaha za nuklia kuanza kutumika miaka ya 1940s.
Akihojiwa na gazeti la Daily Telegraph, Bwana Hague alisema yeye hatopenda kuona suluhu ya kijeshi dhidi ya Iran.
Alisema mataifa ya Magharibi yanafaa kuendelea na sera ya vikwazo vya kiuchumi na chagizo, huku yakifanya mazungumzo na Iran.
No comments:
Post a Comment