Wazazi wa wasichana waliotekwa
nyara nchini Nigeria wamakanusha madai kuwa wanaingiza siasa katika
kilio chao cha kutaka serikali iwaokoe wasichana wao.
Hi ni baada ya wazazi hao kukataa wito wa
kukutana na rais Goodluck Jonathan hapo jana baada ya kushinikizwa na
mwanaharakati mdogo kutoka Pakistan Malal Yousafzai.Bwana Jonathan amesema ni aibu kubwa kwa wazazi hao kuruhusu kushinikizwa na mitandao ya kijamii hasa kutokana na kampeini yao yenye kauli mbiu, "Bring Back Our Girls".
Lakini msemaji wa wazazi hao, (Dauda Iliya) alisema kuwa walikataa kukutana na Rais kwa sababu jamii ya watu wa Chibok haikuwa imewapa ruhusa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment