TANGAZO


Wednesday, April 29, 2015

Rais mstaafu Mkapa, Mama Anna Mkapa, Ujumbe wa Msumbiji waifariji famila ya Brigedia Jenerali Hashim Mbita

Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akimfariji mjane wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Brigedia Jeneral, Hashim Mbita, Ngeme Mbita, wakati alipofika na mkewe, Mama Anna, kuwafariji nyumbani kwa marehemu, Chang'ombe, Temeke jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Igalula, mkoani Tabora, Tatu Ntimizi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe, Mama Anna, wakiwasili nyumbani kwa marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita kuifariji familia ya marehemu Mbita. Kulia ni mtoto wa marehemu Mbita, Idd Hashim Mbita.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akisaini kitabu cha maombolezo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe, Mama Anna, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani hapo jana.
Ujumbe wa Chama cha Frelimo cha Msumbiji, ukiwasili nyumbani kwa marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita kuifariji familia ya marehemu Mbita, ukiongozwa na Mwenezi wa Chama hicho, Raimundo Pachinuapa (mwenye kofia). Kushoto ni Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Vicente Veloso. 
Kiongozi wa Ujumbe wa Chama hicho, Raimundo Pachinuapa, akisaini kitabu cha maombolezo. 
Kiongozi wa Ujumbe wa Chama hicho, Raimundo Pachinuapa akimfariji mjane wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Brigedia Jeneral, Hashim Mbita, Ngeme Mbita.
Kiongozi wa Ujumbe wa Chama hicho, Raimundo Pachinuapa akimfariji mtoto wa marehemu Brigedia Jeneral, Hashim Mbita, Mbita Hashim. Kulia ni Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Frelimo, Damiano Jose, ambaye pia ni Naibu Mwenezi wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment