TANGAZO


Wednesday, July 16, 2014

Maisha jela kwa wabakaji Misri


Mahakama nchini Misri, imewahukumu maisha jela wanaume saba na wengine wawili kifungwa miaka 20 au zaidi kila mmoja kwa kuwabaka wanawake wakati wa sherehe za kutawazwa kwa Rais Abdul Fattah al-Sisi.
Watuhumiwa walipatikana na hatia kwa makosa mengine mengi ikiwemo jaribio la ubakaji na udhalilishaji wa wanawake.
Bwana Sisi aliamuru waziri wake wa mambo ya ndani kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa wa ubakaji na dhuluma nyinginezo za kingono baada ya wanaume hao kukamatwa kwa kuwashambulia wanawake katika medani ya Tahrir.
Duru zinasema kuwa hukumu hiyo, huenda ikaodnoa wasiwasi kuwa maafisa nchini Misri hawachuku hatua kali dhidi ya vuisa vya dhuuma za kingono.
Kulikuwa na ghadhabu miongoni mwa umma baada ya kanda liyomuonyesha mwanamke aliyekuwa uchi akibururwa katika barabara za mji mkuu Cairo.
Kanda hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii.
A court in Egypt has sentenced seven men to life in prison and two others to 20 years for sexual assaulting women last month.

No comments:

Post a Comment